UMASKINI NA UTAJIRI: KATIKA MAWANDA MAPANA YA KITEOLOJIA
Book information
Description
Kitabu hiki kwa mara ya kwanza nilikiandika mwaka 2017 katika lugha ya Kiingereza na kilichapiswa katika mtandano wa Amazon Kindle. Pia nakala ngumu yake inapatikana kwa kuagiza kupitia amazon. Kichwa chake kwa Kiingereza kinaitwa, “THE SCHOOL of POVERTY AND RICHES: A New Hope to the Desperate World. Niliamua kukiandika kwa Kiswahili ili kuruhusu watu wengi kusoma na kuelewa vizuri dhana ya Umaskini na Utajiri; tumaini jipya kwa ulimwengu unaopotoka. Utakubaliana nami kwamba katika ulimwengu huu dhana ya maskini na wanyonge imetawala kiasi kwamba kuwa mnyonge au maskini imekuwa kama ni heshima fulani hivi. Vivyo hivyo, watu kuwa matajiri siku hizi wanahofia kwa kuogopa kwamba pengine labda watu wanafikiri nimewapoka mali zao ndiyo maana nimekuwa tajiri. Yawezekana pia ukakubaliana nami kwamba maskini wengi wamekuwa mitaji ya mitume na manabii; kwa maana ya kwamba maskini wengi ndio ambao huenda kuombewa na kuangushwa na mapepo; (eneo hili bado tunatafiti uhusiano kati ya umaskini na kuangushwa na pepo) lakini huo ndio ukweli. Katika kitabu hiki, nimejadili kwa undani masuala ya umasikini na utajiri kwa kuzingatia muktadha wetu, lakini vilevile nimechukua dhana ya kutangulia kuchaguliwa na kuijadili kwa undani ili kuona kama hatima ya umaskini na utajiri imeamuriwa na Mungu. Karibu tujifunze pamoja Daniel John Seni Januari 2021 Yaliyomo TABARUKU 0 UTANGULIZI 1 SURA YA KWANZA 6 Kwa nini Tuzungumzie mafanikio yanayolenga umasikini na utajiri? 6 Msingi wa kitheolojia kuhusu masuala ya uchumi 13 Nini dhana ya utajiri na umaskini katika jamii tofauti tofauti? 17 Maana halisi ya utajiri kwa mujibu wa maandiko Matakatifu 19 Utajiri ni nini? 20 SURA YA PILI 28 Je Hali Ya Kiuchumi Ya Watu Imetayarishwa? (Predestined?) 28 Je Mipango yetu ya Baadaye Inathirika Vipi Na Dhana Hii ya Kutayarishwa Mapema? 34 Agano la Mungu na Adamu 37 Agano la Mungu na Ibrahim 38 Agano la Waisrael na Mungu (au Agano la Musa) 41 SURA YA TATU 49 Ingawa Mungu Anajua, Lakini Kupanga Ni Kazi Yako Ili Ufikie Malengo Yako 49 Mambo ya kufanya unapotengeneza kesho yako 51 Tengeneza Jina Lako Kwanza Mw. 12:2 51 Chochote Kile Unachokimiliki Hakikisha Kwamba Umekigharimia 54 Usijaribu kuishi maisha yanayokuzidi. I Tim 6:6 57 Thamini kidogo kinachopita mikononi mwako. Yoh. 6:8-12 58 SURA YA NNE 60 Umaskini ni nini? 60 Chanzo cha umaskini 69 Kutokumtii Mungu 69 Kwa sababu ya kudhulumiwa 71 Kwa sababu ya uzembe 74 Mungu anakupima na kukuthibitishia kama utamwacha au hutamwacha 77 Mungu anakutambulisha kwa Shetani 84 Umaskini mwingine ni matatizo ya kiroho tu 85 Magonjwa yaweza kuwa chanzo cha umasikini. 91 Madeni sugu husababisha umasikini usio na kifani. 93 Ulevi kupindukia 98 Sababu mchanganyiko 105 Ni kweli kufa maskini ni ufala? 106 SURA YA TANO 109 Je Kuna Tumaini Lolote La Kutoka Katika Nje? 109 Tufanyaje Sasa 110 Wajibu wa Serikali kuwasaidia masikini 111 Kwa Wanaotaka Kuajiriwa na Walioajiriwa tu 113 1) Hakikisha unakidhi vigezo vya kazi unayotafuta 114 2) Usiwe Mtu wa Kukata Tamaa Mapema 115 3) Uwe jasiri na Ujiamini 116 4) Kubali Ushindani 117 5) Taja moja kwa moja kazi unayotaka kufanya 117 6) Uwe muwazi/ usiwe mwongo 118 7) Kuwa na wapendekezaji wa kuaminika (Referees) 119 8) Omba kazi sehemu nyingi/usiombe kazi sehemu moja tu 120 9) Usilazimishe kupata kazi 120 10) Mwonekano Wako Uwe wa Kuvutia 121 11) Jiajiri mwenyewe ili uwe mwajiri 121 Mbinu za kuilinda kazi yako 122 1) Kuwa na bidii katika kazi 123 2) Epuka kuwa kikwazo kazini 123 3) Epuka Majungu 124 4) Usijaribu kugoma au kushawishi wengine wagome 124 5) Kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzako 125 6) Epuka mapenzi kazini ila uwe na mapenzi na kazi yako 125 7) Usiwe na Mawazo ya Kutafuta Kazi sehemu nyingine 126 8) Usipokee Simu Mbele ya Bosi wako 127 9) Ombea Kazi yako kila siku 128 10) Toa zaka 90% kwa mara ya kwanza na baadaye 10% 129 11. Ongeza Ujuzi wa kazi yako 131 SURA YA SITA 132 Funguo Nne 132 Fungu 1 133 Sawazisha mtazamo wako kuhusu Mungu 133 Fungu 2 137 Tambua mambo ambayo unayoyaweza na yale usiyoyaweza 137 Funguo 3 139 Tambua watu ambao Mungu amewaandaa kwa ajili yako 139 Funguo 4 145 Epuka uchoyo na tamaa ya mali 145 Mwisho 150
Similar books
NIAMUE LIPI? MAADILI YA KIKRISTO
2013 · PDF
MABADILIKO YANAYOUMIZA NDANI YA KANISA
2020 · PDF
NJONI TUABUDU: TARATIBU ZA IBADA (KWA MAKANISA YA KIPRESITERI)
2020 · PDF
WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI)
2020 · PDF
SOTERIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU
2021 · PDF
ANTHROPOLOJIA : MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU MWANADAMU
2021 · PDF
EKKLESIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU KANISA (MTAZAMO WA KIHISTORIA)
2020 · PDF
MISINGI YA IMANI: MAFUNDISHO YA KIBIBLIA KUHUSU IMANI YA KIKRISTO (THE WESTMINSTER CONFESSION OF FAITH AND LARGER CATECHISM)
2020 · PDF