KISWAHILI

NIAMUE LIPI? MAADILI YA KIKRISTO

Book information

Year
2013
Language
kiswahili
Format
PDF
Filesize
453 kB (464189 bytes)
Pages
40\40
Time added
2021-04-06 04:49:30

Description

Dunia nzima inahangaika siku hizi kuhusu suala la maadili. Kwa sasa tunazo changamoto mpya ambazo kanisa halijawahi kuzipitia hata siku moja. Ingawa Neno linasema kwamba mambo yote yanayotokea yalishawahi kutokea, lakini jinsi yanavyotokea ni kwa kiwango cha juu sana. Watu wengi hawaelewi waamue lipi katika maisha yao. Tunashuhudia masuala ya kimaadili ambayo hatuna hakika kama yanaenda kinyume na mapenzi ya Mungu ingawa yako katika mjadala mkubwa, na hapa kutoa hitimisho ni kwenda kinyume na masuala ya kitaaluma yanayofanyiwa utafiti. Kuna mambo kama vile; uvutaji wa sigara, je Biblia imekataza kuvuta sigara? Kuna masuala kama vile ndoa za jinsi moja, je Biblia imekataza? Kuna masuala kama vile unywaji wa pombe, masuala ya kingono ambayo hayako wazi katika Biblia. Hapa ndipo sasa tunapohitaji kitu kinachoitwa “kujua maadili ya kikristo.” Hivi unajua kwamba siku hizi ni jambo la kawaida kwa mkristo kupokea rushwa? Kwa madai kwamba hiyo ni fedha ya shukrani au ya maji? Je kubadilika kwa jina ndio kumehalalisha suala hili? Hivi pia unajua kwamba siku hizi kijana wa kiume/kike kushiriki ngono na mchumba wake ni jambo la kawaida sana? Hata hivyo mtu atakuuliza kwani ni dhambi? Si nitamuoa mwenyewe? Mambo kama haya yanachanganya jamii kwa ujumla. Tunahitaji kuwa na mwongozo wa kuamua katika mambo yetu. Kitabu hiki ni mwongozo mfupi wa maadili ya Kikristo kwa sehemu fulani. Tutaangalia hoja za msingi kwa ujumla halafu tunaweza kutabanaisha nini tufanye sasa katika maisha yetu ya kila siku. YALIYOMO NIAMUE LIPI? 4 MAADILI YA KIKRISTO 5 Maadili ni nini? 5 Maadili binafsi 7 Maadili ya kijamii 7 Chanzo cha maadili ya Kikristo 9 Ufunuo wa Kawaida 10 Ufunuo maalum 10 Neno lililo hai 10 Masuala ya Siasa 13 Kanisa na siasa 14 Hoja za wanaataa kujihusisha na siasa 15 Hoja kwa wale wanaokubali kujihusisha na siasa. 15 Maswali la mjadala: 16 Vita katika agano la kale 17 Vita katika agano jipya 17 Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio wakristo 17 Swali la mjadala 18 Umaskini 18 Rushwa 19 Harambee/fund rising 19 Kuomba msaada kwa wasio wakristo 21 Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni msaada wa mtu. 21 Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano 22 Utasa/Ugumba 23 Chanzo cha utasa/ ugumba 24 Kwa wanaume 24 Kwa wanawake 25 Namna ya kushughulikia ugumba/utasa 26 Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25 27 Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30 27 Talaka 29 Nini sababu ya talaka?. 29 Mitazamo mbalimbali kuhusu talaka 32 Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa? 33 Kileo katika maandiko matakatifu 35 Mkristo na kunywa pombe. 36 Misingi ya mkristo kunywa pombe 37 Misingi ya mkristo kutokunywa pombe 38

Similar books