KISWAHILI

SOTERIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU

Book information

Publisher
Truth Printing Press
Year
2021
ISBN
9789976572636
Language
kiswahili
Format
PDF
Filesize
564 kB (577029 bytes)
Series
Teolojia Pangilifu-2
Volume
1
Edition
1
Pages
154\154
Time added
2021-03-31 06:43:32

Description

Na Mwandishi: Huu ni mfululizo wa masomo katika uwanja wa “Teolojia Pangilifu” (Systematic Theology). Sasa tunashughulikia somo la Soteriolojia, yaani somo linalohusu “wokovu wa mwanadamu.” Siku hizi pengine inaweza kudhaniwa kwamba kila Mkristo anajua maana ya wokovu na upatikanaji wake. Watumishi wengi wasiopenda kujishughulisha huishia kusema “Yesu anaokoa” bila kufafanua maana ya sentensi hii nyepesi na rahisi sana. Ni kweli katika muktadha wa misiolojia tunaweza kutumia sentensi nyepesi kama hizi bila kuzitolea ufafanuzi kwa sababu wale tunaowaambia tunachukulia kwamba hawajui kitu chochote. Siku hizi kuna makanisa yanayojiita, “makanisa ya wokovu” ambayo hudai kuhubiri wokovu wa kweli. Hata hivyo, nimegundua mapungufu mengi katika mafundisho yao kuhusu wokovu kwa kudhania kwamba wokovu ni tukio la sekunde moja. Ama kwa hakika, wokovu ni mchakato; ingawa yawezekana michakato hiyo isipangiliwe vizuri na kuleta maana, lakini bado tunapaswa kujua kwamba wokovu ni mchakato. Mchakato wa kumwokoa mwanadamu unaanzishwa na Mungu mwenyewe na kumaliziwa pia na Mungu mwenyewe. Katika kitabu hiki, kwa namna ya upekee nimejaribu kufafanua kwa undani kuhusu michakato hiyo kwa kuzingatia ufafanuzi wa teolojia iliyoboreshwa (Reformed Theology) Kitabu hiki si kwa wale ambao wameshazaja akili zao mafundisho mbalimbali ya wokovu, na hivyo hawataki kubadilisha mwelekeo na kujifunza upya. Pia kitabu hiki si kwa wazembe, wasiopenda kushughulisha akili zao. Si kwa wale wanaopenda kutafuniwa tu, bali ni kwa wale ambao wanaweza kuvunja mifupa na kuelewa. Ninakutia moyo kwamba unaposoma kitabu hiki unahitaji kusoma katika hali ya utulivu, na kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie ili uweze kuelewa zaidi na zaidi somo hili muhimu. Marejeleo mengi yaliyotumika katika kitabu hiki yanatokana na lugha ya Kiingereza, hivyo basi, kwa wale ambao wana uwezo wa kusoma Lugha ya Kiingereza wanashauriwa kupata baadhi ya nakala za vitabu hivyo kwa sababu ni muhimu sana. Yawezekana katika kitabu hiki ninaweza nisikubaliane na baadhi ya tafsiri ya kambi ya Teolojia Iliyoboreshwa kwa asilimia zote, lakini kwa kweli kwa sehemu kubwa inakubaliana na mafundisho halisi ya Neno la Mungu. Yaliyomo TABARUKU i UTANGULIZI ii Yaliyomo vi SURA YA KWANZA 1 Maana ya soteriolojia 1 Kila Dini Hutafuta Wokovu 4 Hitaji la Wokovu kwa Mwanadamu 7 Mpango wa Wokovu wa Mungu kwa Wokovu wa Mwanadamu 10 Mungu alijua mapema kila kitu 12 Mpango wa Kusudi la Mungu la Milele 19 Wito wa Kupokea Wokovu 21 SURA YA PILI 25 MPANGILIO WA WOKOVU 25 SURA YA TATU 34 KUCHAGULIWA MAPEMA NA KUITWA 34 a. Kuchaguliwa 34 Dhana potofu kuhusu kuchaguliwa mapema 42 Majibu kwa dhana potofu 44 Ni Wateule tu. 46 b. Kuitwa 55 Maswali fikirishi 66 SURA YA NNE 67 KUZALIWA UPYA NA KUHESABIWA HAKI 68 a. Kuzaliwa Upya 68 b. Kuhesabiwa Haki 75 SURA YA TANO 88 TOBA NA UTAKASO 88 a. Toba 88 b. Utakaso 97 SURA YA SITA 103 KUFANYWA WANA 103 SURA YA SABA 111 KUHIFADHIWA, UHAKIKISHO NA KUTUKUZWA 111 a. Kuhifadhiwa 111 b. Uhakikisho 122 c. Kutukuzwa 127 SURA YA NANE 129 TULIP 129 T-Total depravity (Upotovu Kamili) 130 U-Unconditional election (Uchaguzi usiokuwa na masharti) 132 L-Limited atonement (Upatanisho wenye Mipaka) 133 I-Irresistible grace (Neema Isiyoweza Kuzuiliwa) 134 P-Perseverance of the saints (Uvumilivu wa Watakatifu) 135 Marejeleo 138

Similar books