Huduma za Afya na Utunzaji wa Watoto
Book information
Description
Huduma za Afya na Utunzaji wa Watoto ni kitabu kinachotoa maelezo muhimu juu ya ulinzi wa afya za watoto na akina mama. Kitabu hiki kimetungwa kwa madhumuni ya kuwasaidia wazazi ili wajisaidie wenyewe na wawasaidie watoto wao katika mambo yahusuyo magonjwa ya watoto wadogo. Matatizo mengi ya kiafya na magonjwa ya watoto wadogo yanaweza kutatuliwa mapema na vizuri zaidi nyumbani. Ili watoto wadogo wapate afya njema na hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na maradhi, inabidi wazazi waelimishwe katika utunzaji wa afya za watoto wao. Inatumainiwa kuwa baada ya kusoma kitabu hiki, wazazi wataweza kutoa huduma za kwanza kwa watoto wao kabla ya kuwapeleka kwa waganga. Vilevile, inatarajiwa kuwa baada ya kusoma kitabu hiki vijana wote wataweza kusaidia sana wazazi wao katika kutoa huduma za kwanza za dharura kwa wadogo zao wanapougua ghafla huko majumbani. Aidha kitabu hiki kitawasaidia sana wafanyakazi wa tiba hasa wakunga, wauguzi wasaidizi, wauguzi wa vijijini n.k. katika kutoa huduma bora zaidi.
Similar books
"Mau Mau" kizuizini: kisa cha miaka saba ndani ya kampi za kuhamishwa katika Kenya
1965 · PDF
Hali ya Haki za Watoto Tanzania: Taarifa ya Utafiti Juu ya Hali Halisi ya Kisheria na Kiutendaji
Koja La Lugha
1969 · PDF
Kamusi ya Watoto
2011 · PDF
Biashara ya Utumwa katika Afrika ya Magharibi
1974 · PDF
Kumbukumbu za Vita vya Maji Maji: Sehemu ya Kwanza, 1905-1907
1967 · PDF
Wanawake wa TANU. Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955-1965
2005 · PDF
Fani ya Fasihi Simulizi kwa Shule za Upili
2011 · PDF