III: Afrika Kuanzia Karne ya Saba Hadi ya Kumi na Moja
Book information
Description
Kipindi kinachojadiliwa katika Juzuu la III kimezingatia uhamiaji wa aina mbili ambao ulikuwa na umuhimu mkubwa na wa kudumu kwenye historia ya Afrika. Athari ya Uislamu ilikuwa inaongezeka upande wa kaskazini na magharibi; ilikuwa ikiingiliana na utamaduni asilia wa Kiafrika. Upande wa kusini kulikuwa na upanukaji wa WaBantu. Kitabu hiki kwanza kinaweka Afrika katika muktadha wa historia ya dunia mwanzoni mwa karne ya saba, kabla ya kuchambua athari za upenyaji wa Kiislamu, kuendelea kwa upanukaji wa watu wanaozungumza Kibantu, na ukuaji wa ustaarabu kwenye kanda za Kisudani za Afrika Magharibi. Sura zinazojadili kwa undani zinafuata zikizungumzia nasaba mfululizo za Kiislamu za Afrika Magharibi na mawasiliano mapana ya nasaba hizo na sehemu zingine, Unubi ya Wakristo, staarabu za savana, maeneo ya misitu na Pwani ya Afrika Magharibi, Pembe ya Afrika, Pwani ya Afrika Mashariki na bara, Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika, na maendeleo ya ndani ya Madagaska pamoja na mawasilino ya Kimataifa. Sura tatu za hitimisho zinafuatilia utawanyikaji wa Waafrika huko Asia, zinachunguza uhusiano wa kimataifa na usambaaji wa teknolojia na mawazo ndani ya Afrika, na kupima athari ya jumla ya kipindi hicho kwa historia ya Afrika.
Similar books
"Mau Mau" kizuizini: kisa cha miaka saba ndani ya kampi za kuhamishwa katika Kenya
1965 · PDF
Hali ya Haki za Watoto Tanzania: Taarifa ya Utafiti Juu ya Hali Halisi ya Kisheria na Kiutendaji
Koja La Lugha
1969 · PDF
Kamusi ya Watoto
2011 · PDF
Biashara ya Utumwa katika Afrika ya Magharibi
1974 · PDF
Kumbukumbu za Vita vya Maji Maji: Sehemu ya Kwanza, 1905-1907
1967 · PDF
Wanawake wa TANU. Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955-1965
2005 · PDF
Fani ya Fasihi Simulizi kwa Shule za Upili
2011 · PDF